Karibu Amago semina blog, ujipatie elimu ya ujasilia mali Tanzania,Leo tutajifunza jinsi ya kutengeneza sabuni ya majivu ya pumba ngumu za mpunga, sabuni hii ni Kwa ajili ya kuoshea vyombo, jinsi ya kutengeneza, chukua ndoo moja ya pumba ngumu za mpunga, zichome moto hadi ziwe majivu meupe pe, baada ya hapo yasage sage hayo majivu mpaka yawe unga mlaini, (3) yachekeche ili kuondoa pumba ngumu au uchafu mwingine kama vile mawe mawe, (4) chukua sabuni ya unga (Omo) kilo tatu (3kg) ichanganye na huo unga wa majivu yako hayo uliyo yaandaa, changanya hadi sabuni na majivu yachanganyikane vizuri zaidi, (5) weka vijiko viwili vya chapa maandashi kwenye mchanganyiko wako huku ukichanganya taratibu kwa mkono Kwa muda wa dakika tatu, (6) mimina matone matano ya pafyumu ndani ya huo mchanganyiko wa sabuni yako huku ukichanganya kwa mkono ili isije ikafanya mabonge kwenye mchanganyiko wako. (7) Anika kidogo kimvulini mchanganyiko wako angarau Kwa muda wa dakika 15 hivi, tayari sabuni yako itakuwa iko tayari kwa kufungashwa na kuingizwa sokoni. Mimi ni wako mwal. Andrew Mago ❤️mpaka hapo utakuwa umeelimika vyakutosha, nikutakie ufualiaji mwema wa makala zinazofuata.